- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
MKUU wa Wilaya ya Lushoto, Mhe. Japhari Kubecha amekabidhi Madume 20 ya Ng’ombe bora wa mbegu aina ya Boran kwa vikundi 20 vya wafugaji wa Tarafa ya Umba yaliyotolewa na serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Kata za Lunguza, Mng’aro na Mnazi.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Ng’ombe hao iliyofanyika katika Mnada wa mifugo uliopo katika Kata ya Lunguza Mhe. Kubecha alisema kwamba lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuinua ustawi wa wafugaji kwa kufanya ufugaji wenye tija wa kufuga mifugo michache yenye faida kubwa.
Mhe. Kubecha alivitaka vikundi hivyo vya wafugaji kuhakikisha vinatunza Ng’ombe hao kwa hali zote na kuwaendeleza ili baada ya muda idadi yao iongezeke na kuwafikia wafugaji wengi zaidi na kufanikisha azama ya Mhe. Rais, Dkt Samia.
Aliendelea kusema kwamba vikundi vitakavyonufaika na Ng’ombe hao vihakikishe vinazingatia miongozo iliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto kuhusiana na mradi huo wa madume ya mbegu bora na lolote watakalotaka kulifanya lazima wafanye mawasiliano na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Mhe. Kubecha alitumia fursa hiyo ya kukabidhi Ng’ombe hao wa mbegu, kumshukuru, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe pamoja na Mbunge wa Jimbo la Mlalo, Mhe. Rashid Shangazi kwa kufakikisha uwepo wa mradi huo.
Katika hatua nyingine; Mhe. Kubecha alisema kwamba Ng’ombe hawa wasiwe chanzo cha migogoro badala yake alisisitiza kwamba ni muda sahihi kwa jamii ya Wafugaji na Wakulima kushikamana na kuendena na sera ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha Amani inatawala katika kila eneo kwa sababu Mhe. Rais. Dkt. Samia hapendi migogoro.
Akizungumzia kero ya Tembo, Mhe. Kubecha, alisema Serikali inatambua kero hiyo na inafanya kila jitihada kuhakikisha inatokomeza jambo hilo na kuwapa uhuru wananchi kufanya shughuli zao za uzalishaji bila vikwazo.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa