- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Katibu mwenezi wa CCM Mh.Sofia Mjema afanya ziara fupi katika wilaya ya Lushoto na kutembelea Jengo la mama na mtoto ambalo liko katika hatua ya usafi ili lianze kutumika, Wakati wa ziara hiyo ameahidi kufatilia suala la watumishi watakao hitajika ili kituo hicho kiweza kuanza kufanya kazi kuanzia 1/3/2023. Pia alisema kwamba serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Rais Dk Samia Suluhu imetoa bilioni 900 kwa ajili ya kuandaa mashamba ya vijana ili waweze kujiajili kwenye kilimo cha kisasa. Kwahiyo amewaimiza vijana kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kujiajili kwenye kilimo ili waondokane na umasikini.Kuhusu barabara katibu mwenezi kitaifa amesemea serikali Mama Samia imeishotoa pesa kwa miradi yote inayotekelezwa katika wilaya ya lushoto ni utekelezaji tu ikiwemo mradi wa barabara wa Magamba Mlola kwa kiwango cha rami.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa